© TIB Development Bank 2019 | Disclaimer | Terms and Conditions | Staff Mail

UZINDUZI WA BARAZA LA WAFANYAKAZI TIB

Baraza la wafanyakazi Benki ya Maendeleo TIB lilizinduliwa rasmi siku ya tarehe 30 November 2018.

Uzinduzi huo ulifunguliwa rasmi na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi  Dkt. Mary Mashingo ikishuhudiwa na Mkurugenzi Mkuu Bw. Charles Singili, Wakurugenzi wa Idara na wawakilishi wa wawafanyakazi kutoka idara mbalimbali.

Uwepo wa baraza hili unaratajiwa kuleta mabadiliko makubwa ikiwa ni pamoja na kuimarisha ushirikiano kati ya menejiment na wafanyakazi. Ni ni kuongeza ufanisi na uwajibikaji kazini.

“Nipende kuwakumbusha kwamba ni wajibu wa kila mfanyakazi wa Benki ya TIB kuhakikisha anafahamu na kutimiza wajibu wake mahali pa kazi, anatekeleza malengo aliyopangiwa katika muda uliopangwa, vile vile anatunza mali na vifaa alivyokabidhiwa kufanyia kazi. Wajibu huo ni pamoja na kuwahi kazini, kufanya kazi kwa uaminifu na uadilifu ili kulinda sura ya Benki.” aliasa Mwenyekiti wa Bodi alipotoa hotuba yake wakati wa uzinduzi huo.

Mchakato wa uzinduzi wa baraza TIB ulianza tangu mwaka jana (2017) na mkataba wa kuanzisha baraza  ulisainiwa  tarehe 10 Aprili 2018 baina ya Menejimenti ya TIB na Menejimenti ya TUICO, na mnamo tarehe 12 Aprili 2018 Mkataba huo uliridhiwa na Kamishna wa kazi.

Katika uzinduzi huo iliundwa kamati tendaji ya baraza  ikijumuisha wajumbe sita.