Karibu Benki ya Maendeleo TIB

Mikopo ya Viwanda

Sekta ya viwanda ni moja ya sekta muhimu ambayo inachangia Pato la Taifa (GDP) kwa kutoa ajira kwa   Watanzania wengi wanaofanya kazi katika viwanda vidogo na vya kati. Sekta ya viwanda ni kichocheo cha ukuaji wa maeneo mengine ya kimkakati ili kuleta mabadiliko ya kiuchumi kutoka hali ya kipato cha chini inayotegemea kilimo hadi uchumi shindani kupitia uwekezaji katika sekta za viwanda na huduma.

Benki inalenga kutoa mikopo ya viwanda katika maeneo yafuatayo:

    - Usindikaji wa mazao ya kilimo

    - Uchimbaji na uchakataji wa madini ghafi

    - Uzalishaji wa bidhaa mbalimbali.

Sifa za mkopo

    - Kugharamia viwanda vipya na viwanda vinavyohitaji kuongeza uwezo wa uzalishaji

    - Kipindi cha rehema (grace period) wakati wa ujenzi wa viwanda au uagizaji wa mitambo

    - Riba nafuu

    - Ili kuepuka changamoto za mabadiliko ya thamani ya fedha za kigeni mikopo hutolewa kulingana na fedha ya mapato ya mradi

    - Muda mfupi katika kupitia maombi ya mkopo.

Faida za mkopo

    - Kumwezesha mteja kupata vifaa na mashine bora zenye uwezo wa kutumika kwa muda mrefu

    - Kuwezesha kufikiwa kwa ndoto za mteja za kumiliki kiwanda ndani ya muda mfupi

    - Kumuunganisha mteja na benki za biashara kwa ajili ya kupata mkopo wa muda mfupi (overdraft) ili kuwezesha uzalishaji kuanza

    - Ushauri kutoka kwa watalaamu mbalimbali wa benki, wakiwemo wahandisi wa viwanda

    - Kuwezesha kampuni / taasisi kuwekeza bila vikwazo vingi

    - Kuhamasisha shughuli za maendeleo ya biashara na uchumi kwa ujumla, ili kuchagiza maendeleo ya kitaifa.

Mikopo ya Viwanda : Mfano wa kiwanda cha kuchakata mazao ya Kilimo

blog