Mikopo ya Miundombinu
Benki ya Maendeleo TIB imetengeneza mkakati wa kushirikiana na serikali katika jitihada za kukuza maendeleo ya uchumi kwa kuwekeza katika miundombinu mbalimbali ikiwemo ya usafiri, nishati, maji, mafuta, gesi na sekta mawasiliano. Ujenzi wa miundombinu ni muhimu hasa pale nchi inapofikia uchumi wa kati ikiwa ni jitihada za kuboresha utoaji wa huduma muhimu kwa wananchi.
Katika mkakati wa benki ujenzi wa miundombinu ili kuwezesha utoaji wa huduma kwa jamii; benki inatoa mikopo ili kuimarisha sekta hii katika nyanja zifuatazo:
Miradi ya kitaifa:
Hii ni miradi ambayo utekelezaji wake huleta matunda kwa nchi nzima. Miradi hii inaendelezwa na serikali kupitia mashirika yake au wakala wa serikali (TANROADS, TARURA, TCAA n.k). Miradi ya miundombinu inayoweza kupatiwa mikopo ya aina hii ni pamoja na:
- Huduma za umeme, maji na mawasiliano; ufuaji wa umeme na usambazaji, usafishaji wa maji na usambazaji, mindombinu ya gesi na mafuta na TEHAMA.
- Usafiri: ununuzi wa vichwa vya treni na mabehewa, ujenzi na upanuzi wa bandari, viwanja vya Ndege na reli.
- Ununuzi wa vifaa vya usafirishaji: meli, ndege, mabasi, na vyombo vingine vya usafirishaji.
Miradi ya ubia kati ya sekta ya umma na sekta binafsi:
Upanuzi wa miundombinu ufanywa pia kwa ubia kati ya sekta binafsi na sekta ya umma (PPP). Benki hutoa mikopo kuwezesha sekta binafsi kushiriki katika miradi ya namna hii.
Sifa za mkopo
- Mikopo hii hutolewa kwa riba nafuu.
- Mikopo hii ni ya kipindi cha muda mrefu wa marejesho unaofikia mpaka miaka ishirini (20).
- Kipindi cha rehema (Grace period) hii hutolewa kulingana na aina ya mradi.