Mikopo ya Wawekezaji Wadogo na Wakati
Katika kutimiza moja ya malengo yake makuu ya kimaendeleo, Benki ya Maendeleo TIB inalenga kukuza wajasiriamali na wawekezaji wadogo na wakati kwa kutoa aina mbalimbali za mikopo maalumu. Mikopo hii inalenga kuongeza na kukuza upatikanaji wa fedha kwa wajasiriamali hawa pamoja na kukuza shughuli zao na kuboresha mazingira yao ya kibiashara.
Benki inatoa mikopo mbalimbali kwa ajili ya SMEs ili kukidhi mchango wake katika kusaidia shughuli za maendeleo na kukuza biashara.
Benki ya Mandeleo TIB inatoa mikopo kwa vikundi/wajasiriamali waliosajiliwa (kama kampuni au vyama vya ushirika) na vyenye rekodi nzuri za biashara.
Huduma kwa wajasiriamali zitolewazo na benki ni pamoja na:
- Mikopo ya moja kwa moja kwa vikundi/wajasiriamali waliosajiliwa.
- Ukukopeshaji kwa ajili ya programu mbalimbali za wajasiriamali na maendeleo ya miundombinu ya viwanda.
- Mikopo kwa ajili ya wakopeshaji waliosajiliwa kutoa huduma za kifedha kwa wajasiriamali.
- Mikopo ya maandalizi ya maandiko ya miradi na ushauri wa kitalaamu juu ya miradi mbalimbali.
Faida za mkopo
- Ulipaji unaoendana na mzunguko wa kibiashara / mtiririko wa fedha wa mradi.
- Mikopo ya SMEs inatolewa kwa ajili ya uwekezaji ikiwemo ujenzi na ununuzi wa mitambo pamoja na kiasi cha kuanzia shughuli za awali za uendeshaji.
- Husaidia taasisi za kibinafsi na za umma uwekezaji mpya na upanuzi wa biashara.
- Mikopo ya SMEs inawezesha taasisi za kibinafsi na za umma kufikia matokeo ya miradi inayotarajiwa kwa haraka.
- Benki inatoa msaada wa kiufundi katika kuandaa miradi kwa taasisi za umma.
- Mikopo hii ni ya muda mrefu na kipindi cha ulipaji kufikia hadi miaka 10 ambayo ni muhimu katika uwekezaji.
- Kipindi cha rehema (grace period) cha mkopo hutolewa kulingana na aina ya mradi.
- Mkopaji atachangia angalau 40% ya jumla ya gharama za uwekezaji kulingana na uwekezaji uliopo na wa ziada.
- Riba za mikopo hii ni nafuu.